- Wanaowajibika kuhiji.
- Waislamu wenye sifa zifuatazo wanalazimika kuhiji;
- Waliobaleghe – Watoto wadogo hawawajibiki kuhiji hata kama wana uwezo,
hata hivyo wanaruhusiwa chini ya uangalizi wa wazazi wao.
- Wenye Akili timamu – Asiye na akili timamu hawajibikiwi kwa ibada yeyote
ile katika Uislamu.
- Waungwana – Wafungwa au watumwa hawawajibiki kwa Hijja mkapa
watakapokuwa huru.
- Wenye uwezo – Waislamu wote wenye uwezo kimali na afya njema ni wajibu
kutekeleza ibada ya Hijjah.
- Wasio katika kizuizi – Waliowekewa kizuizi au kuzuiliwa kwa sababu za
kiusalama sio wajibu kwao kuhiji muda huo.
- Wanawake waongozane na maharimu wao.
- Mwanamke mwenye uwezo atawajibika kuhiji iwapo ataongozana na
maharimu wake.