Kwa mujibu wa Qur’an (9:60) na (2:273), wanaostahiki kupewa Zakat ni waislamu tu katika makundi yafuatayo;

  1. Fukara.

-    Ni kundi la wale wasiojiweza kwa chochote cha kumudu maisha yao kabisa ya kila siku bila kusaidiwa.

 

  1. Maskini.

-    Ni wale wasio na uwezo wa kupata mahitaji yao ya msingi ya kimaisha ila wana uwezo wa kujikimu kwa kiasi fulani tu.

 

  1. Wanaozitumikia (Al-A’miliina A’laihaa).

-    Ni wale wote wanaozikusanya na kuzigawanya kwa wanaohusika bila kujali uwezo wao.

 

  1. Wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.

-    Ni wale walioingia katika Uislamu karibuni na wanahitajika kuimarishwa imani zao juu ya Uislamu.

 

  1. Kuwakomboa Watumwa (Fir-riqaabu).

-    Ni kuwakomboa au kuwanunua watumwa au watu wote wanaoishi chini ya miliki ya watu (mabwana) na kuwaachia huru.


 

  1. Kuwasaidia wanaodaiwa kulipa madeni yao.

-    Ni kuwalipia waislamu madeni yao waliokopa ili kujikimu kimaisha lakini bila kukusudia wameshindwa kulipa deni zao.

 

  1. Kutumika Katika njia ya Allah (s.w).

-    Ni kutumika katika shughuli zote zinazopelekea kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.

 

  1. Kuwasaidia Wasafiri walioharibikiwa njiani (Ibnis-sabiil).

 -    Msafiri yeyote muislamu aliyeharibikiwa kwa kupoteza, kuibiwa au kuishiwa mali yake hata kama ni tajiri, ni wajibu kupewa zakat.