Ishara na Dalili za mtoto mwenye pepopunda ;

1. misuli ya taya kukaza.
2. Ugumu wa shingo
3  Ugumu wa kumeza chakula,maji au chochote kutokana na shingo kuwa ngumu.
4. Ugumu wa misuli ya tumbo.
5. Homa.
6. Kutokwa na jasho.
7.  Kuongezeka kwa shinikizo la damu
8. Kiwango cha moyo au mapigo ya moyo kuenda haraka.
8. Kutokuwa na uwezo wa kunyonya .

 
 Yafuatayo ni matatizo ya pepopunda;

1  Ugumu kwenye  kamba za sauti ni shida ambayo inaweza kusababisha kuingiliwa kwa kupumua.
2. Kuvunja uti wa mgongo au mifupa mirefu kutokana na degedege.
3. Shinikizo la damu
4. Mdundo usio wa kawaida wa moyo.
5. Maambukizi ambayo ni ya kawaida kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu hospitalini.

 

 Namna ya Kuzuia pepopunda kwa watoto chini ya miaka mitano;
1. Hakikisha Mtoto amepata dozi za pepopunda
2. Kuhimiza kujifungua katika kituo cha afya.
3. Mafunzo sahihi kwa wakunga wa jadi .
 4.Kampenia za elimu ya afya kuelekea utunzaji sahihi na safi wa kisiki cha kitovu, ziara za baada ya kuzaa na kuangalia kitovu wakati Mtoto amezaliwa.
4. Ukaguzi wa vifaa na njia inayotumika katika kushughulikia kitovu wakati wa kujifungua.
5. Chanjo kwa wanawake wa umri wa kuzaa zifike dozi tano.
6. Wanawake wote wajawazito ikiwa hawajamaliza dozi 5 wanapaswa kuchanjwa angalau dozi 3 (hata dozi moja ni bora kuliko kutofanya chochote.)