. Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.
- Mfumo wa Mapato na Uchumi katika Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah.
Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah ilipata mapato yake kupitia njia zifuatazo;
- Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali (Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.
- Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.
- Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.
- Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.
- Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.
- Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.
- Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.