Katika Tajwid, Miim Saakinah ina hukumu maalum zinazoeleza jinsi ya kutamka herufi hiyo inapokutana na herufi nyingine. Hukumu hizi ni muhimu ili kuhakikisha kuwa Qur'an inasomwa kwa usahihi na ufasaha. Hukumu za Miim Saakinah ni:

 

1. Idghaam Shafawi (الإدغام الشفوي)

Idghaam Shafawi hutokea pale Miim Saakinah inapokutana na Miim nyingine. Hapa, Miim ya kwanza huingizwa kwenye Miim ya pili pamoja na ghunnah (sauti inayotokea puani).

Mfano:

2. Ikhfaa Shafawi (الإخفاء الشفوي)

Ikhfaa Shafawi hutokea pale Miim Saakinah inapokutana na herufi Ba (ب). Hapa, Miim itafichwa na kutamkwa kwa ghunnah.

Mfano:

3. Idh'har Shafawi (الإظهار الشفوي)

Idh'har Shafawi hutokea pale Miim Saakinah inapokutana na herufi yoyote isiyokuwa Miim au Ba. Hapa, Miim itatamkwa kwa uwazi bila ya ghunnah.

Mfano:

 

Mwsho:

Katika somo linalofuata tutakwendakujifunza kuhsu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid.