Swali:

Samahani naomba kuhuliza je unaweza kutokwa na maji maji ambayoa ayana rangi Wala harufu Ni dalili gani kwa mimba ya mwezi mmoja

 

Jibu:

Majimaji yasiyo na harufu wa rangi ya tofauti na kawaida, ukiwa na ujauzito majimaji haya hayana tatizo. Kawaida mwili wa mwanamke una njia ya kukinga njia ya uzazi dhadi ya mashambulizi ya bakteria ambayo yangeweza kuathiri mtoto tumboni. Hivyo majimaji haya husaidia katika kulinda njia ya uzazi iendelee kubakia salama na madhubuti dhadi ya mashambulizi ya bakteria, fangasi na vijdudu vingine.

 

Vyema kufika kituo cha afya endapo  majimaji haya yatakuwa na harufu mbaya, ama yana rangi tofauti na kawaida ama yakiwa yanawasha.