Sababu za kuharibika kwa figo.

1. Kuchelewa kwenda haja.

Mtu anapohisi mkojo na akautunza bakteria uanza kuhama kutoka kwenye kibofu cha mkojo na kuanza mashambulizi kwenye figo kwa hiyo pindi tusikiapo mkojo nenda ukakojoe.

 

2.Kula chumvi kupita kiasi.

Pia hili nalo ni tatizo ambalo Usababisha kuharibika kwa figo kwa kawaida kila siku Tunapaswa kula chumvi kiasi cha gramu tano na pointi nane na zikizidi tunaweza kupata matatizo ya figo kwa hiyo ni vizuri kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula.

 

3.Kula nyama kupita kiasi .

Kuna Watu wenye tabia ya kula nyama kupita kiasi na kuongeza kiasi kikubwa cha protini kwenye mwili  ambacho uharibu figo kwa hiyo tunapaswa kula nyama kwa kiasi kidogo sio kila siku nyama hasa nyama nyekundu.

 

4.Unywaji wa kupita kiasi kwa vinywaji vyenye caffeine, kama vile soda na kahawa , kwa hiyo tunywe vinywaji hivi ila kwa kiasi kidogo sana hasa wale wenye umri wa magonjwa nyemelezi wanapaswa kupunguza sana.

 

5. Kutokunywa maji 

Hili nalo ni tatizo ambalo Usababisha kuaribika kwa figo kwa sababu maji yanahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kusaidia kusafisha uchafu uliopo kwenye figo na uchafu ukiwa mwingi unasababisha kuaribika kwa figo