Static property ni nini
Kama ilivyo static method basi na static property ni property ambayo inaweza kutumiaka moja kwa moja bila ya iinstance of class.
Hapa nitakupa mifano miwili tena, kwanz ani property ambayo sio static na mfano wa pili ni property ambayo ni static. Bila shaka utapata kuelewa vyema. Hata hivyo hakuna utofauti na static method.
<?php
class gari {
public $jina = 'Toyota';
}
$myob = new gari();
echo $myob->jina;
?>
Kama tulivyoona kwenye static method basi hata kwenye static property tunatumia scope operator (::) ili kuweza kuitumia
<?php
class gari {
public static $jina = 'Toyota';
}
echo gari::$jina;
?>
Endapo static property itatumika ndani ya class basi tutatumia keyword self kama tulivyoona kwenye static method.
<?php
class gari {
public static $jina = 'toyota';
public function tangazo() {
return 'tunauza gari aina ya '. self::$jina;
}
}
$myob = new gari();
echo $myob->tangazo();
?>
Pia kama static method itatumika kwenye child class, tutatumia keyword parent
<?php
class gari {
public static $jina = 'Toyota';
}
class toyota extends gari {
public function tangazo() {
return 'tunauza gari aina ya '. parent::$jina;
}
}
$myob = new toyota();
echo $myob->tangazo();
?>
Mwisho
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifundisha kuhusu namespaces