Swali:
Nivipi nafasi ya elikuvkatika uislamu?
Jibu:
- Nafasi ya Elimu katika Uislamu.
- Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika Uislamu inaonekana katika maeneo yafuatayo;
1. Elimu ndio takrima ya kwanza aliyopewa mwanaadamu na Mola wake kama nyenzo pekee itakayomuwezesha kumjua Mola wake na kumuabudu vilivyo.
“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya (fani za) vitu vyote” (2:31) na pia rejea (2:38).
2. Elimu ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu kuitafuta kama alivyoamrishwa kusoma Mtume (s.a.w).
“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba……..” (96:1-5).