Maumivu wakati wa hedhi 

1.Haya ni maumivu ambayo uwapata wanawake walio wengi na wasichana kwa kawaida huwa katika makundi mawili, kuna maumivu ambayo utokea wakati wa hedhi na maumivu haya huwa hayaambatani na magonjwa yoyote ila kuna aina ya pili ambapo maumivu utokea ni kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa kwenye via vya uzazi.

 

2.kuna sababu za kuwepo kwa maumivu wakati wa hedhi ni pamoja na matatizo kwenye mfuko wa kizazi kwa sababu kama kuna Maambukizi kwenye mfumo wa kizazi lazima Maumivu yatakuwepo au pengine panakuwepo na uvimbe kwenye mfuko wa kizazi ambao usababisha maumivu wakati wa hedhi.

 

3.Pengine maumivu kwenye mfuko wa uzazi Usababishwa na msongo wa mawazo  kwa sababu unakuta kuna wanawake wengine wanaishi mazingira magumu na kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi kwa hiyo tunapaswa kupunguza msongo wa mawazo ili kuepuka mawazo mbalimbali Ambayo yanaweza kusababisha maumivu wakati wa hedhi.

 

4.Maambukizi kwenye mlango wa kizazi.

Kwenye mlango wa kizazi panaweza kuwepo kwa Maambukizi kama kuna Maambukizi kuna Maambukizi ndiyo usababisha maumivu wakati wa hedhi mara nyingine panaweza kuwepo viashiria vya kansa ya mlango wa kizazi au pengine Maambukizi kutokana na ngono zembe kwa hiyo kama kuna mambo kama hayo Maumivu wakati wa hedhi ni kawaida.

 

5.Kwa hiyo tunapaswa kujua kubwa kwa wale wenye maumivu makali wakati wa hedhi wanapaswa kwenda hospitalini kupima ili kuangalia shida ni nini ambayo inafanya kuwepo kwa maumivu hayo kwa hiyo tunapaswa kuepuka na msongo wa mawazo ili tuweze kuepuka matatizo ya kuwa na maumivu wakati wa hedhi.