Zoezi la 6.
- (a) Ainisha idadi ya sura za Makkah na za Madinah.
(b) Tofautisha kati ya sura za Makkah na zile za Madinah.
- Onesha jinsi ambavyo Qur’an iliwekwa katika msahafu moja wakati wa Mtume (s.a.w) na umuhimu wa kunakiliwa upya wakati wa Uthman bin Affan (r.a).
- Bainisha hoja za Makafiri dhidi ya Qur’an na udhaifu wa hoja hizo.
- (a) Kwa kurejea Suratul-Fiyl, andika tafsiri yake na kisha toa mafunzo matano yatokanayo na sura hiyo.
(b) “Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo, asengenyaye, msengenyaji” (104:1).
Kwa mujibu wa aya hii, dhihirisha ubaya wa kusengenya.
- “Kisha mtaulizwa juu ya (kila) neema mlizoneemeshwa” (102:8).
Kwa mujibu wa aya hii, bainisha baadhi ya neema alizopewa mwanaadamu na Mola wake.
- Eleza hatua alizochukua Mtume (s.a.w) katika kuihifadhi na kuilinda Qur’an.