Mambo hayo ni haya:-
1. Kusoma Qur'ani Tukufu
Ni jambo linalopendeza kwa mwenye udhu kusoma Qur'ani Tukufu. Ingawa kusoma Qur'ani bila udhu kunaruhusiwa kwa mujibu wa wanazuoni wengi, kuwa na udhu wakati wa kusoma Qur'ani ni bora zaidi na ni katika kuheshimu Kitabu cha Allah.
2. Kusoma Hadithi na Elimu za Dini
Mwenye udhu hupendeza kujishughulisha na kusoma hadithi za Mtume ﷺ, tafsiri ya Qur'ani, fiqhi na elimu nyingine za Kiislamu. Hali ya twahara huongeza utulivu na heshima kwa elimu ya dini.
3. Kumdhukuru Allah
Miongoni mwa mambo yanayopendeza kwa mwenye udhu ni kumkumbuka Allah kwa tasbihi, tahmidi, takbiri na aina mbalimbali za dhikri.
Allah amesema:
"Basi nikumbukeni, nami nitawakumbuka."
(Al-Baqarah: 152)
4. Kumswalia Mtume ﷺ
Ni jambo jema kwa mwenye udhu kuzidisha kumswalia Mtume Muhammad ﷺ, kwani kufanya hivyo ni sababu ya kupata rehema na baraka kutoka kwa Allah.
5. Kukaa Msikitini Kusubiri Swala
Mwenye udhu akikaa msikitini akisubiri Swala huwa katika ibada na hupata malipo makubwa mbele ya Allah.
Mtume ﷺ amesema:
"Malaika humwombea mmoja wenu maadamu yuko mahali pake pa kuswalia, mradi hajapata hadathi."
(Sahih Al-Bukhari na Muslim)
6. Kuhudhuria Vikao vya Elimu
Ni jambo linalopendeza kuhudhuria darsa, mawaidha na vikao vya elimu ukiwa katika hali ya udhu. Hii ni katika kuipa elimu heshima yake.
7. Kulala Ukiwa na Udhu
Ni katika sunnah kutia udhu unapokwenda kulala. Kutia udhu napokwenda kulala kunaweza kukupa ulinzi wa Allah.
8. Kudumu Katika Udhu
Miongoni mwa sifa za Waumini wema ni kujitahidi kubaki katika hali ya udhu mara nyingi iwezekanavyo.
Faida za Kudumu na Udhu
-
Huongeza ukaribu kwa Allah.
-
Humwandaa Muislamu kwa Swala wakati wowote.
-
Huongeza usafi wa mwili na moyo.
-
Humpatia Muislamu utulivu na nuru Siku ya Kiyama.
Hitimisho
Muislamu anatakiwa kupenda kuwa katika hali ya udhu kadiri anavyoweza. Kusoma Qur'ani, kufanya dhikri, kuhudhuria vikao vya elimu, kukaa msikitini na kulala akiwa na udhu ni katika mambo yanayopendeza na yanayomletea thawabu nyingi. Hivyo, ni vizuri kujizoesha kudumu katika twahara ili kupata radhi za Allah na kufuata mwenendo wa Mtume ﷺ.