Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya Ki-Ilhamu
- Hatuna budi kuwaandaa watoto wetu kuwa Makhalifah (viongozi) wa Allah (s.w) hata kabla hawajazaliwa.
- Hatuna budi kuwaandaa walimu (madai’yah) watakaoufundisha Uislamu na taaluma zingine kwa lengo la kuusimamisha Uislamu katika jamii.
- Hatuna budi kushirikisha familia zetu kwenye harakati za kuuhuisha na kuusimamisha Uislamu katika jamii.
- Wanawake wa Kiislamu hawanabudi kumuiga Bi Khadija, mkewe Mtume (s.a.w) katika kuwasaidia waume zao katika harakati za kuupigania Uislamu.
- Pia hatuna budi kuchukia kila aina ya uovu na dhuluma unaofanywa katika jamii, na tujitahidi kuyaondoa kwa mikono na kauli zetu kabla ya kujitenga.
- Hatuna budi pia kujipamba na kila tabia na mwenendo mwema kwa kadri ya uwezo wetu.
- Pia hatuna budi kujiimarisha kiuchumi kwani ndio ni katika nyenzo kuu za kuweza kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.