Mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito.
1.Kwanza kabisa tunajua wazi kuwa mama akibeba mimba na mzunguko wa damu unabadilika kwa sababu hapo awali ni Mama pekee aliyekuwa anatumia damu ila kwa sababu ya kuwepo kwa kiumbe kingine ili nacho kiweze kutunzwa kwa miezi tisa na msukumo wa damu ubadilika kama ifuatavyo.
2.Moyo.
Kiasi cha moyo ubadilika kwa asilimia kumi na mbili kwa hiyo kiasi cha moyo uongezeka ili kuweza kusukuma damu kwa mama na kwa mtoto hali hii ya mabadiliko uchukua miezi tisa na baada ya miezi tisa hali huwa kawaida.
3.Mapigo ya moyo nayo uongezeka.
Wakati wa ujauzito na mapigo ya moyo ubadilika yaani uongezeka kutoka kwa asilimia themanini na tano mpaka asilimia hamsini, hali hii utokea ili kuweza kusukuma damu kwenye figo, ubongo na katika mishipa mingine ya damu.
4. Spidi ya damu nayo uongezeka.
Spidi ya damu uongezeka kutoka kwenye kiwango cha kawaida kwa sababu uweza kusukuma damu kwa haraka kutoka kwa Mama ili kuweza kuondoa wadudu wanaoweza kusababisha magonjwa na pia kuweza kuweza kusafirisha mahitaji yote kwa mtoto na Mama.
5. Kiwango cha seli nyeupe za damu nacho uongezeka ili kuweza kuzuia kuwepo kwa bakteria na kupambana na Maambukizi yoyote ambayo yanaweza kushambulia Mama na mtoto wakati wa ujauzito.
6. Kwa hiyo akina Mama wakisikia mabadiliko kwenye miili yao wanapaswa kufahamu kubwa ni kwa sababu ya kuwepo kwa mimba na baadae hali inakuwa kawaida