- Kuandaliwa Muhammad (s.a.w) kabla ya kupewa Utume.
- Maandalizi (mafunzo) haya yalikuwa ya Kiil-hamu ambayo hata Muhammad mwenyewe na jamii haikujua kuwa anaandaliwa, na yalikuwa kama ifuatavyo;
- Kuzaliwa katika kabila tukufu la Kiqureish ambalo ni kizazi cha Nabii Ibrahim (a.s) kupitia kwa Nabii Ismail (a.s).
Rejea Qur’an (2:129).
- Kupewa jina la Muhammad na babu yake lililo na maana sawa na ‘Ahmad’- Mshukuriwa, alilotabiriwa nalo katika Injili, na Qur’an pia.
Rejea Qur’an (61:6).
- Malezi bora aliyopata kupitia Mama yake mzazi, Bi Halimah, babu yake Abdul-Muttalibu na Ami ya Abu Talibu pamoja na kuwa alikuwa yatima.
Rejea Qur’an (93:6).
- Tabia yake njema isiyo na mfano kuanzia utotoni hadi utuuzima wake kutoathiriwa na kila aina ya ubaya.
Rejea Qur’an (68:4).
- Ndoa yake Muhammad (s.a.w) na Bi Khadija bint Khuwailid, aliiandaa Allah (s.w) ili kumuwezesha Muhammad kuitumikia jamii hata kabla ya utume.
Rejea Qur’an (93:8).
- Kuchukia kwake maovu na kujitenga pangoni ili kutafuta msaada ulio nje ya uwezo wa kinaadamu baada ya kufanya jitihada mwisho wa uwezo wake.
Rejea Qur’an (93:7) na (94:1-3).