Swali:

Habari za asubuhi doctor. Naomba msaada wako.....je siku ya kwanza kabisa ya ovulation mimba inakuwa ni uhakika?

 

Jibu:

Mimba huigia wakati mwanamke yupo katika siku hatari tu.  Hata hivyo haimaanishi kuwa ndio lazima utapata ujauzito pindi ukifanya tendo katika siku hizi. Kuna mambo mengi yanaweza kusababisha mimba usipate hata kama umeshiriki katika siku hatari.

 

Mambo yanayozuia ujauzito:

1. Mbegu kuwa chache

2. Mbegu kuwa dhaifu

3. Kuzidi kwa tindikali kwenye mirija ya falopia

4. Kuwepo na vizuizi vitakavyozuia mbegu zisilifikie yai

5. Mbegu kuwa changa yaani hazijakomaa

6. Yai kutokukomaa vyema

 

Hivyo asi unaweza basi kwa sababu hizi unaweza kushiriki tendola ndoa bila ya kinga katika siku hatari na usipate mimba.