Swali:  

habari ninapenda kujua kuwa endapo mama atafanya tendo la ndoa wiki moja kabla ya kuingia hedhi anaweza kupata ujauzito?

 

Jibu: 

Haiwezekani,  kwani muda huo anakuwa nje ya siku hatari.  Kawaida yai la mwanamke hutolewa kati ya siku 14 hadi 16 kabla ya kuingia hedhi yake inayofuata.

 

Katika makadirio hapo unaweza kupata kuwa wiki moja kabla ya kuingia hedhi ipo nje ya siku hatari,  hivyo hawezi kupata mimba.