- Funga za Sunnah na namna ya kutekeleza.
- Kufunga siku tatu kila mwezi.
- Ni kufunga siku tatu mfululizo za mbalamwezi, mwezi 13, 14 na 15.
- Kufunga ya siku ya Jumatatu na Al-khamisi.
- Jumatatu ni siku aliyozaliwa Mtume (s.a.w) na Al-khamisi ni siku kupandishwa amali za mja kwenda kwa Mola wake.
- Kufunga siku sita za mwezi wa Shawwal.
- Ni kufunga sita mara baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha.
- Funga ya Arafa.
- Ni kufunga siku ya mwezi 9, Dhul-Hijj ambamo mahujaji wako katika kisimamo katika uwanja wa Arafa.
- Funga ya Ashura.
- Ni kufunga siku ya mwezi 10, Muharram (mfungo nne). Ni siku aliyookolewa Nabii Musa na Bani Israil kutoka kwa utawala wa Firaun.
- Funga katika mwezi Shaaban.
- Ni kufunga kwa wingi katika mwezi wa Shaaban bila ya kutimiza siku 30.