Katika somo hili tutakwenda kutumia mifano yetu ya somo lililotangulia ili kuweza kujienga uelewa zaidi.

 

Jinsi ya kuandika switch case

switch(expression){

Case value:

Code

break

}

 

Ukiangalia hapo ni kuwa utaanza na keyword switch  utaweka mabano () kama kawaid ndani yake ni value tunayotaka ku test ikufuatiwa na mabano {}. Kisha utaweka keyword case ikifuatiwa na sharti unayotaka ku test kisha utawka nukta pacha ( : ). Baad aya hapo ni code ambazo zita run kisa utaweka keyword break kwa akiji ya ku stop code zisiendelee ku run

 

Wacha tuone mambo yanavyokuwa:

Tunataka ikiwa umri wa mtoto ni miaka 7 aambiwe aende shule.

void main() {

 var umri = 7;

 switch(umri){

   case 7:

     print('aende shule');

     break;

 }

}

 

 

Sasa tunataka kama ni chini ya kiaka 7 aambwe hajafika umri, na kama miaka 7 aambiwe aende shule, na kama ni  miaka 13 au zaidi aambiwe aende mmemkwa. Tutakwenda ku test miaka 10

void main() {

 var umri = 10;

 switch(umri){

   case <7:

     print('aende chekechea');

     break;

 

   case ==7:

     print('aende shule');

     break;

 

   case >=13:

     print('aende memkwa');

     break;

 }

}

 

Hapo utaona hakuna matokeo yeyote. Ni kwa sababu 10 haopo kwenye test zetu. Kwahiyo hapo tunatakiwa kuweka default yaani tuweke code ambazo zitafanya kazi ikiwa sharti hata moja halijafikiwa.

 

Sasa tunataka ikiwa hakuna sharti lolote lililofikiwa basi iseme umesha je umesoma?

void main() {

 var umri = 10;

 switch(umri){

   case <7:

     print('aende chekechea');

 

   case ==7:

     print('aende shule');

     break;

 

   case >=13:

     print('aende memkwa');

     break;

 

   default:

     print('je umesoma?');

 }

}

 

Hakuna ukomo wa kutumia switch case unaweza kutumia zaidi na zaidi. Miongoni mwa fgaida zake ni kuwa ni rahisi kuitumia, na inapunguza mrundikano wa code nyingi kuliko kwenye if else else if.