Method ni nini?

Method ni kama function tofauti ni kuwa method zina mahusiano makubwa na object. Hapa nitakuletea baadhi tu ya method zinazotumika kwenye string:-

 

1. String length

Hii hutumika katika kujuwa je string ina character ngapi.

void main(){

 String text = "haloo bongoclass";

 print(text.length);

}

Hii itakupa jibu 16 kumaanisha hapo kuna herufi (character) 16

 

2. Kubadili herufi kuwa ndogo au kubwa

kubadil i kuwa herufi ndogo utatumia  toLowerCase     na kubadili kuwa kubwa utatumia toUpperCase

void main(){

 String text1 = "haloo bongoclass";

 String text2 = "HALOO BONGOCLASS";

 print(text1.toUpperCase());

 print(text2.toLowerCase());

}

HALOO BONGOCLASS

haloo bongoclass

 

3. Kuigawa string kwenye (substring)

Kwa mfano katika neno bongoclass tunataka kuprint neno bongo tu. hapo tutaangalia hilo bongo linapatikana kutka characterya ngapi hadi ya ngapi

void main(){

 String text = "bongoclass";

 print(text.substring(0, 5));

}

bongo

 

4. Kuchuja string (contains)

Kwa mfano unahitaji kuangalia kama je neno fulani lipo ama halipo kwenye string.  Kama lipo utapata jibu true na kama halipo jibu ni false. Wacha tuangalie je neno class lipo kwenye neno bongoclass?

void main(){

 String text = "bongoclass";

 print(text.contains('class'));

}

true

 

5. Kubadili string kuwa list data type (split)

Hapa tutakwenda kuigawa string kwenye mafungu. Kw amfano neno haloo karibu bongo class. Tutagawa kwa kila neno

void main(){

 String text = "haloo karibu bongoclass";

 print(text.split(","));

}

void main(){

 String text = "haloo karibu bongoclass";

 print(text.split(' , '));

}

[haloo karibu bongoclass]

 

6. Kubadili list kuwa string (join)

void main(){

 var text = ['haloo karibu bongoclass'];

 print(text.join(','));

}

haloo karibu bongoclass

 

  1. Kuangalia je string imeanzia ama kuishia na neno fuani.

Kwa neno katibu bongoclass hapa tutakwenda kunagalia je string yetu imeanza na neno bongoclass kama kweli jibu true na kama si kweli jibu ni false

void main(){

 String text = 'karibu bongoclass';

 print(text.startsWith('bongoclass'));

 print(text.endsWith('karibu'));

}

false

false

 

8. Kuondoa nafasi za ziada.(trim)

void main(){

 String text = '   karibu bongoclass   ';

 print(text);

 print(text.trim());

 print(text.trimLeft());

 print(text.trimRight());

}

 

9.  Kubadili sehemu ya string

Kwa mfano badala ya kusema karibu bongoclass tunataka kubadili neno karib kuwa kwaheri.

void main(){

 String text = '   karibu bongoclass   ';

 print(text.replaceAll('karibu', 'kwaheri'));

}

kwaheri bongoclass


 

Mwisho

Hizi method zipo nyingi sana. Hivyo unaweza kuzitafuta nyingine kwenye tutorial mbalimbali. Katika somo linalofuata tutakwenda kunagalia method ambaz hutumika kwenye namba.