Utangulizi

Css ni kifupisho cha maneno cascading style sheet. Hii ni moja katika lugha za kompyuta ambazo hutumika katika kuboresha mtindo kwenye ukurasa wa wavuti. Hutumika kwenye HTML na XML. css ni style sheet angauage, hata hivyo haipo pekee kwenye kundi hili. Lugha nyingine za style ni kama:

 

Css ilianzishwa miaka ya 1990 na kuendelea. Historia a css imeanza punde tu baada ya tovuti ya kwnza kuchapishwa na watu wakaanza kutengeneza tovuti mbalimbali. Hivyo ikaonekana kunahitajika kuwepo na ubireshwaji wa muonekano.

 

Mwaka 1994 ndipo css ilianzishwa rasmi na Håkon Wium Lie na Bert Bos. Kutokea hapo css iliweza kukuw kwa kasi. Na kuanza kupata u maarufu. Mpaka sasa tupo toleo la 4 la css.

 

Kama nilivyotangulua kusema kuwa css hutumiaka kwenye HTML na xml katika course hii tutakwenda kujifunza kutumia css kwenye html. Tutajifunza kutumia style sheet kwneye xml kwenye course ya xml.

 

JINSI YA KU INSTALL CSS

Hakuna uhitaji wa ku install css ili uweze kuitumia kama zilivyo lugha nyingne. Unachotakiwa kufanya ni kuitumia moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa wavuti kwenye html. Kuna njia kadhaa ambazo hutumika katika kutumia css kwenye faili la HTML. Njia hizo ni kama:-

  1. In line css: Hapa tuna andika css ndani ya mstari katika  faili la html.
  2. Internal css Hapa tutatumia css ndani ya faili la html.
  3. External css Hapa tunaandika css kwenye faili lingine kisha tuna iunganisha moja kwa moja
  4. Kwa kutumia javascript Katika njia hii tunanaitumia css kenye code za javascript.

 

Katika course hii tutakwenda kutumia njia hizo tatu za kwanza. Njia ya nne tutatjifunza kwenye course ya javascript level 1 na level 2.

 

In line css

Njia hii utakuwa na uzoefu nayo kwani tumesha itumia mara kadhaa kwenye course yetu ya html level  1 na level 2. Njia hii ni ile ya kutumia tag za css kwenye fali la html. Tag yenye we ni ile ya <style>. Kwa  kutumia tag hii ndani ya html itakuwezesha kuweza kuandika code za css na zikaweza kufanya kazi.

 

Katika inline css tutaandika css ndani ya tag ya html kw akuanza na neno style likifatiwa na attribute zake. Tutakwenda kutumia code hizi kwenye mfano huu:-

<html>

<head>

    <title>Bongoclass</title>

</head>

<body>

<p>Karibu bongoclass</p>

</body>

</html>


 

Mfano 1:

Tunataka kubadili nano karibu bongoclass kuwa na rangi ya buluu. Tutafanya hivi kwa kutumia in line css. Unachotakiwa kufanya ni kuweka style ndani ya tag ya <p>, ikifuatiwa na alama ya = kisha utaweka hizo attribute za css kwenye alama za kunukuu (“).

 

Uandishi wa attribute utakuwa hivi, kwanza utaweka jina la property likifuatiliwa na nukta pacha (:) ama colon, Kisha utaandika value. Mfano ikitaka rangi iwe ya buluu utaweka style="color:blue" katika mfano huo hapo neno color ndio property na neno blue ndio value.

 

Hivyo tag ya html <p>itasomeka hivi <p style ="color:blue">Karibu bongoclass</p>

 

Pia unaweza kuweka style zaidi ya Moja kwenye inline css. Kufanya hivyo utatenganisha style Moja na nyingine kwa kutumia alama ya semicolon yaani  (;).

 

Mfano 2:

Katika mfano wetu huu tunataka kufanya maadhishi yawe makubwa kwa asilimia 200%. Kufanya hivi tutatumia property ya font-size kwa kuwa tunayo property ya color basi tutatenganisha kwa semicolon

 

<p style ="color:blue; font-size:200%">Karibu bongoclass</p>

 

Internal css

Tunapotumia internal css hapa tunaweka code zote za style sehemu Moja. Mara nyingi code hizo huwekwa sehemu head kwenye faili la html. Na code hizo za css huwa kwenye tag ya <style>

 

Katika internal css code za css zitakuwa ndani ya mabano {}. Tutakuja kujifunza Sheria zaidi za css kwenye somo linalofuata.

 

 

Katika mfano wetu wa hapo juu code hizo kwenye internal css zitakuwa hivi:-

 

<style>

      p{

        color:blue;

        font-size:200%

      }

</style>

 

Code zote zitakuwa hivi:-

<html>

  <head>

    <title>bongoclass</title>

    <style>

      p{

        color:blue;

        font-size:200%

      }

    </style>

  </head>

  <body>

    <p>Karibu bongoclass</p>

  </body>

</html>

 

External css 

Katika mtindo huu tutaweka code za css mbali na faili la html. Kwanza tutatengeneza faili la css, kisha tutakuja kuliunganisha na html. Kwenye kifaa unachotumia tengeneza faili ipya liite style.css. Kisha weka code hizo tulizoweka kwenye internal css ila kusiwepo na hizo tag za style.

 

 

Utaona hapo kwenye folda langu kuna mafaili mawili ambayo ni index.html na faili la style.css. Hili la index ndlo ambalo litakaa code za html na hili la style ndilo ambalo litakaa code za css. Kama nilivyokwambai hapo pest code zetu tulizotumia hapo juu

 p{

        color:blue;

        font-size:200%

    }

 

Kwenye faili la css code zetu zitaonekana hivi:-

 

Sasa tunakwenda kuunganisha mafaili yetu haya mawili ili code za css ziweze kutumika kwenye faili la index.html. Ili kufanya hivi tutatumia tag ya <link> ambayo itakuwa na attribute ya rel hii kazi yake ni kuonyesha uhusiano uliopo kati ya faili na faili lingine. Neno rel ni kifupisho cha neno relation. Katika tag ya kink kuna attribute nyingine kama type  na href

 

Katika rel tutaweka property ya stylesheet kuonesha aina ya hilo faili tutalotaka kuliunganisha kwenye faili letu la html. Mfano rel=”stylesheet”. Katika type tutaweka MIME type ama format ambayo ni text/css mfano type=”text/css” na katika href tutaweka link ama location ama path ya hilo faili la css. Mfano href=”style.css” kwa kuwa mafaili yote yapo kwenye folder moja.

 

Hivyo basi tag nzima ya <link itasomeka hiv

<link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css"> 

 

Code nzima za faili la html ztasomeka hivi

<html lang="sw">

<head>

    <title>Bongoclass</title>

    <link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css">

</head>

<body>

<p>Karibu bongoclass</p>

</body>

</html>

 

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu sheria za uandishi wa css.